WATANZANIA wameshauriwa kujenga tabia ya kudai bidhaa zenye ubora
toka nje ya nchi, hususan China ili kukomesha uingizwaji wa bidhaa zisizo na
viwango.
Rai hiyo imetolewa kutokana na
malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu kuzagaa sokoni kwa
bidhaa kutoka China zisizokidhi viwango vya ubora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na
Kilimo (TCCIA),
Daniel Machemba, alisema hayo juzi katika mkutano wa maandalizi
ya maonyesho ya China Afrika, yanayotarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Daniel mchemba |
Machemba aliwataka wafanyabiashara wanaonunua bidhaa kutoka China,
wasikubali kutengenezewa bidhaa zisizo na ubora kwa lengo la kujipatia faida
kubwa kwa vile kufanya hivyo ni kuwaumiza
watumiaji.
"Tanzania inapaswa kuiga mfano wa nchi za Ulaya, ambazo
zimekuwa zikitumia bidhaa kutoka China, lakini zenye viwango vya juu vya ubora
kutokana na msimamo wao wa kutotaka zisizo na ubora," alisema.
Alisema biashara kati ya Tanzania na China ni muhimu kwani tangu
mwaka 2001, Tanzania imekua ikiuza bidhaa nyingi nchini humo, zikiwemo
zisizokubalika sehemu nyingine duniani.
Mwakilishi wa Uchuni na Biashara wa Ubalozi wa China nchini, Wang
Fang, akizungumza katika mkutano huo, alisema kwa sasa serikali ya China
inafanya kila iwezalo kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa Tanzania zinakuwa
na ubora wa hali ya juu.
Alisema kampuni zitakazoshiriki katika maonyesho hayo ni za kiwango
cha juu nchini China, hivyo aliwahakikishia Watanzania ubora wa bidhaa
zitakazouzwa mahali hapo kuwa ni wa uhakika.
No comments:
Post a Comment