Na mwandishi wetu
VIONGOZI wa dini wameaswa kuendelea kufanya ibada za kimwili na kiroho kwa waumini ili kuwajengea maadili mema.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya jamii na kupunguza matukio ya uhalifu na kwamba, viongozi hao wana nafasi kubwa ya kuhakikisha hilo linatekelezwa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Ernest Mangu, alisema hayo jana wakati alipokutana na kuteta na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
shaaban bin simba |
Mkutano huo uliowahusisha baadhi ya Masheikh wa mikoa nchini, Kadhi wa Zanzibar pamoja na Maimamu wa misikiti, ulifanyika jana kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Alisema haijawahi kutokea duniani kwa polisi kula njama na viongozi wa dini katika kupambana na uhalifu na kuwataka kuongeza mahubiri kwenye nyumba za ibada ili jamii iweze kutenda mema.
Pia alisema kwa kupitia nyumba za ibada, jamii na viongozi waimarishe kamati za ulinzi ili kuhakikisha amani inakuwepo maeneo yote ya ibada.
Kwa upande wake, Mufti Simba alisema dini zote zinahimiza waumini kutenda mema na kujiepusha na vitendo viovu.
Amelitaka jeshi la polisi kuendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanaotenda uhalifu kwani, hata kwenye taasisi za dini nako kuna uhalifu.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Arusha, Shabani Juma, wakati akitoa salamu za mkoa huo, alisema hali kwa sasa ni shwari na amani, hivyo wana wajibu wa kulinda amani tuliyonayo.
No comments:
Post a Comment