Arnaud Montebourg (kulia) akiwa na Benoit Hamon |
PARIS, Ufaransa
RAIS Francois Hollande ametangaza kulivunja baraza la mawaziri baada ya kuibuka msuguano miongoni mwa mawaziri.
Aidha, amemtaka Waziri Mkuu Manuel Valls aliyetangaza kujiuzulu, kuunda baraza jipya kabla hajaondoka kwenye kiti hicho.
Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya Ikulu Ufaransa vilisema kuvunjwa kwa baraza hilo kunatokana na kutofautiana kimtazamo kwa mawaziri kuhusu uchumi wa nchi.
Rais Hollande alimtaka Valls kuunda baraza jipya kabla ya kuondoka katika nafasi yake jambo ambalo linatafsiriwa kuwa huenda viongozi hao walikubaliana kuhusu uamuzi huo.
Mapema jana Valls alitangaza kujiuzulu wadhifa wa waziri mkuu kutokana na kile alichosema ni shutuma za baadhi ya mawaziri ndani ya baraza hilo dhidi ya sera ya uchumi.
Valls alimshutumu Waziri wa Uchumi, Arnaud Montebourg kwa kuikosoa serikali hadhari licha ya yeye mwenyewe kuwa sehemu ya watekelezaji wa sera hiyo.
Mbali na waziri huyo mwingine anayetoa upinzani dhidi ya serikali katika baraza hilo ni Waziri wa Elimu, Benoit Hamon ambao kwa pamoja wanatarajia kuachwa katika uteuzi mpya.
Hammon amekuwa akiishutumu Ufaransa kwa kufuata sera za uchumi zinazopangwa na Ujerumani jambo alililosema halitasaidia maendeleo ya taifa.
No comments:
Post a Comment