WANACHAMA wajasiriamali wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), jimbo la Ukonga, wametakiwa kuwa wabunifu wa kukuza mitaji wanayopatiwa kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ujasiriamali.
Diwani wa Kata ya Msongola, Angela Malembeka, alitoa mwito huo
juzi katika mkutano wa makatibu wa UWT uliofanyika Kata ya Ukonga, Dar es
Salaam.
Angela pia alikabidhi msaada wa sh. milioni nne kwa wanawake
wajasiriamali wa kata nane za jimbo hilo, ambapo kila kata imepatiwa sh. laki
500,000.
Kata zilizopatiwa fedha hizo ni Msongola, Ukonga, Chanika, Pugu,
Majohe, Gongo la Mboto, Kitunda na Kivule
Angela alisema kiasi hicho cha fedha alichokitoa kwa wanawake hao
ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya kuwawezesha wananchi
wake, hususani wanawake.
Alisema awali, wajasiriamali hao walipatiwa mafunzo yakiwemo ya
kutengeneza batiki, vikoi na chaki, lakini tatizo lilikuwa katika kupata mitaji
ya kufanya shughuli walizosomea kwenye kozi mbalimbali za ujasiriamali.
Licha ya changamoto zinazowakabili wanawake hao, ikiwemo ya kukosa
mitaji ya uhakika, Angela alisema wanakabiliwa na changamoto ya masoko ya
kudumu ya kuuzia bidhaa zao, hivyo alizitaka mamlaka zinazohusika kuwasaidia
kupata soko.
No comments:
Post a Comment