Friday, 15 August 2014
MADAI YA NDOA YA JIDE KUVUNJIKA , GARDNER AFUNGUKA
HABARI kubwa ya mjini hivi sasa , hasa kwenye
mitandao ya kijamii ni juu ya madai mazito ya
kuvunjika kwa ndoa ya selebriti wawili Bongo, staa
wa muziki wa Kizazi Kipya , Judith Wambura ‘ Lady
Jaydee ’ au ‘ Jide ’ na mtangazaji maarufu wa Radio
Times FM , Gardner G . Habash , iliyofungwa Mei 14,
2005, Ijumaa linamaliza utata .
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya , Judith Wambura
‘ Lady Jaydee ’ au ‘Jide ’ akiwa na mumewe Gardner
G . Habash wakati wa harusi yao.
KABLA
Kabla ya Gardner kufunguka , habari zilidai kwamba
wawili hao walikuwa kwenye gogoro zito ambapo
Gardner aliamua kuondoka katika nyumba
waliyokuwa wakiishi pamoja iliyopo Kimara -
Temboni , Dar .
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka nyumbani eti
Gardner alikwenda kukaa kwa mmoja wa ndugu
zake.
Habari hizo za kwenye mitandao ambazo hazitaji
chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo , zilidai watu
wa karibu na familia hiyo walisema hiyo siyo mara
ya kwanza kwa wawili hao kutengana , lakini mzozo
wa safari hii unaweza ukawa wa moja kwa moja.
ACHA BWANA !
Ilidaiwa kwamba ni kutokana na kutemana huko,
ndiyo maana Jide msanii anayetajwa kuwa ni
miongoni mwa wenye mafanikio kimaisha Bongo,
hakwenda Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar
kumwangalia mumewe ambaye aliwekwa korokoroni
kufuatia kitendo chao cha kuwakimbia askari wa
usalama barabarani akiwa na Ephraim Kibonde hivi
karibuni .
Maselebriti , ‘Lady Jaydee ’ au ‘ Jide’ na Gardner G .
Habash wakipata ukodaki kwenye Red kapeti.
MAFUMBO?
Ilisemekana kuwa hisia za kuachana huko
zinachochewa pia na baadhi ya maandiko ambayo
mwanamuziki huyo wa Kibao cha Yahaya , amekuwa
akiyaweka katika akaunti zake za mitandao katika
siku za hivi karibuni .
Ilielezwa kwamba katika akaunti yake ya Mtandao
wa Istagram, Jide aliweka picha yake akiwa
amesimama nje ya gari lake kisha akasindikiza kwa
kuandika hivi : “Walking away from troubles”,
maneno ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi
yanamaanisha kujiondoa kwenye matatizo .
BINTI MACHOZI?
Ilidaiwa kuwa kabla ya hapo , katika mitandao
inaandikwa kuwa Jide pia aliweka picha yake
akionekana kuwa na huzuni huku Binti Machozi
akilengwalengwa na machozi na kusindikizia na
maneno akiuliza : “Sijui nisemaje ?”
IJUMAA MZIGONI
Kufuatia tetesi hizo , gazeti hili liliamua kuzifanyia
kazi ili kupata ukweli.
GARDNER ANASEMAJE?
Mtu wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni Gardner
ambaye aliipokea na kabla hajaelezwa chochote,
alisema alikuwa katika sehemu ambayo asingeweza
kuzungumza, hivyo angempigia mwandishi wetu
baada ya robo saa.
JIDE VIPI?
Baada ya kukata simu, mwandishi wetu alimwendea
hewani Jide na baada ya kuita kwa muda , simu
yake ilipokelewa na Gardner akasema: “Mpigie
baada ya robo saa. ”
‘Lady Jaydee ’ au ‘ Jide’ akipozi .
DAKIKA 20 BAADAYE, GARDNER AFUNGUKA
Dakika ishirini baadaye , Gardner alimtumia ujumbe
mfupi wa simu mwandishi wetu na kumweleza kuwa
alikuwa Kituo cha Polisi Oysterbay , Kinondoni jijini
Dar ambako aliitwa kwa ajili ya soo lao la
kuwakimbia trafiki.
Baada ya kubadilishana maneno kadhaa, baadaye
aliamua kupiga na mazungumzo kati yake na
Ijumaa yalikuwa kama ifuatavyo ;
Ijumaa : Ebwana hivi hizi habari kwenye mitandao
juu ya kuvunjika kwa ndoa yako na Jide zimekaaje?
Gardner: Hamna kitu bwana, watu wanaunganisha
tu vitu sijui kwa sababu gani.
Ijumaa : Sasa kama ni hivyo kwa nini Jide hakuja
kukuona siku ile ulipolala polisi ?
Gadner : Unaona sasa , wao wanajua hivyo , lakini
siyo kweli , Jide alikuja usiku sana kwa sababu
alikuwa anawaogopa mapaparazi .
Unajua Jide yeye huwa hapendi hayo mambo .
Alikuja usiku sana, lakini hata hivyo polisi nao
walimgombea sana kumpiga picha.
Ijumaa : Wanasema Jide kuna maneno amepost
kwenye akaunti zake mitandaoni zinazoonyesha
kuchoshwa na wewe , unasemaje?
Gardner: Si ndiyo kama hivyo nimekuambia , watu
wanaungaunga tu vitu ambavyo hawavijui na sisi
hata hatujui malengo yao.
Wakati ule uliponipigia simu mara ya kwanza
nilikuwa naye kwenye gari ananipeleka pale polisi ,
lakini akapaki mbali kwa sababu hiyohiyo
niliyokuambia kuogopa mapaparazi na si
unakumbuka hata ulipompigia kwenye namba yake
nilipokea mimi ?
Ijumaa : Kwani upo naye hapo sasa hivi nimsalimie?
Gardner: Hapana tumeachana mimi niko kwenye
usafiri mwingine naelekea kazini na yeye yupo
kwenye misele mingine .
Ijumaa : Haya kaka basi poa .
Gardner: Poa kaka , mchana mwema .
HUKO NYUMA
Si mara ya kwanza kwa mastaa hao kudaiwa
kutibuana kwani walisharipotiwa kutaka kutengana
lakini mara nyingi huwa wanakaa chini na
kuyamaliza kimyakimya .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment