Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar , hivi
karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa
kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake
aitwaye Mama Sofia , kisa kikidaiwa ni mume wa
mtu.
Mbuva, akiwa na majeraha usoni baada ya
kumwagiwa mafuta ya moto.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita
ambapo inadaiwa mama Sofia alimfanyia mwenzake
unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana
wake.Akisimulia ilivyokuwa , Mbuva alisema : “Mama
Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa
safarini eti nilitembea na bwana wake.
“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita kwake,
nilikuwa sipajui ila akanielekeza , ile nafika tu
majirani zake wakamwambia mimi ndiye nilikuwa
nakwenda kulala pale na mume wake. “Nikajaribu
kujitetea lakini hakunielewa . Nikaondoka , baadaye
akaniita tena , kufika pale nikakuta ugomvi kati ya
mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia
akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto
akanimwagia usoni.
“Nikaanza kupiga kelele , watu wakajaa ndipo
tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha
Polisi cha Mazizini na tukaandikisha , mimi
nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu uso wangu bila
kosa , Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni
hapahapa duniani .”
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja
kuzungumzia tukio hilo.
Imeandikwa na Shani Ramadhani , Mayasa
Mariwata na Rhoda Josiah.
No comments:
Post a Comment